Wednesday 14 October 2009

Upumzike salama mwalimu Nyerere

Leo ni siku ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu. tarehe 14 october. Nakumbuka mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tukiomba sala Nyerere hasife hii tarehe lakini ikashindikana akafa. Tulikuwa tunamaliza darasa la saba ilikuwa siku ya sherehe. Tulizuiwa tusipige ngoma wala mziki, basi wapiga mziki tulokuwa tumela tumewakodisha walikula pesa yetu tu bure. Duh kweli nimekuwa kubwa miaka 10 sasa tangu nimalize darasa la saba ahhah lakini bado ninasoma tu.

Upumzike salama mwalimu daima ifikapo siku kama ya leo ntakukumbuka na naimani wote tuliomaliza darasa la saba au asilimia 90 tuliguswa sana na kifo cha mwalimu.

Tuesday 13 October 2009

Unene unapokuvamia







Jamani mwenzenu nilivamiwa na unene baada ya kupata mimba.
Wakati niko bk miezi 6 kbl sijaolewa nilikuwa hivi(Picha namba moja kutoka chini)

nikajitupa gym kidogo (Picha namba 2)

Nilipojifungua nkawa hivi (Picha namba 3)
Kuona nimekuwa hivi kidogo nikawa nimépunguza mazoezi nikafanya kula tu nikarudi tena nikawa hivi (picha namba nne) hivi sasa niko hivi hapo utuonapo famili ila nataka nipungue kidogo tena so nimeanza gym tena, vifaa vichache ninavyo home ila nashindwa kufanya mwenywe so nimeamua niende gym mwezi hivi ili niweze kujijengea mazoea.

Nahunganika na dada Dina kupunguza miili hii make mili mikubwa hifadhi za magonjwa.