Tuesday 4 August 2009

SIMLIZI (UPENDO WA MAMA

Habari za leo na karibu katika kigoda chako tayari kunisikiliza leo nimekuletea nini, ni tarehe moja mwezi wa saba mwaka 2009 saa kumi na mbili na dakika 26 kwa saa za skandinavia na saa moja za kibongo. Namshukuru Mungu kunionyesha siku ya leo Namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto BYERA ambaye leo ninasherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake miaka mitatu na masaa dunia, Asante Mungu. Leo nataka niongelee juu ya UPENDO WA MAMA, Kama rafiki yangu mpendwa alivyonishauri, ni rafiki nimpendaye sana na sijui kama itakuwaje… Nilimuuliza siku moja nikitafuta ushauri wa hadithi gani nitunge akaniambia nitunge juu ya upendo wa mama, sasa nafanya hivyo, najisikia kichwani kitu kimekaa tayari kuandikwa. Haya karibuni.
 
 
 
Je kati yangu na wewe ninani alipokuwa mdogo angependa kutoka shule akapokelewa na maneno km haya, mbwa wewe mbona umechelewa ulipitia wapi, shika ndoo hapo ukimbie kisimani ukateke maji kisha uwapikie wadogo zako chakula, mi naenda kwa mama koku kumjulia hali, kwanza nakueleza we nani, fanya haraka mbona unanitumbulia macho kama mjusi kabanwa na mlango, nasema timua. Bila hata ya kupewa chakula, kupewa muda wa kupumzika hata kumuona mdogo wako mwenye umri wa miaka 5 mliyeondoka wote asubuhi wakati anaenda kwenye shule yake ijulikanayo kama vidudu au chekechea.
 
Natambua kila mmoja wetu angetamani kupokelewa na upendo na tabasamu la kutosha pindi atokapo shule, kuulizwa mwanangu ilikuwaje, leo umesoma nini na kadharika. Kwa ukarimu kuisikia sauti ya mama yako mzazi ikikwambia karibu mtoto mzuri, nipe busu kisha ukavue nguo za shule, mi ngoja nikakuandalie chakula ule kisha upumzike kidogo. Hakika huo UPENDO wa namna hiyo unapatikana asilimia 100 kwa mtu mmoja aitwaye MAMA.
Mwanamke kama mwanamke naomba utambue kwanza kabla ya kuendelea kuwa uchungu ulioupata wakati unajifungua KAMGISHA AU KAGEMLO ni ule ule alioupata MAMA KOKU wakati akiwazaa KOKU na NDYAMKAMA. Hauna uzito tofauti na wako wala hauna rangi. Hii ilitokana na EVA kulila TUNDA alilokatazwa na Muumba wetu kwamba asile, na tokea hapo MUNGU alisema wewe mwanamke utazaa kwa uchungu. Hivyo uchungu huo niwakila mwanamke azaaye so SHOGA zangu msiwe na roho za kwa nini nakujiona watoto wenu ndio wanafaa. Haya karibu kigodani.

Itaendelea...

UJUMBE WA LEO: Kutoa ni moyo si utajiri, saidia yatima, mjane, maskini yeyote aliyekaribu yako, na MUNGU ATAKUBARIKI. Nawapenda

No comments:

Post a Comment