Monday 31 August 2009

Namshukuru Mungu

Binadamu sisi niwasahaulifu sana. Utakuta mtu anaamka asubuhi anakurupuka kitandani mbio bila hata kumwomba Mungu ulinzi wala kumshukuru Kwa ulinzi wote usiku ule alipokuwa ameuchapa usingizi. Binadamu tujifunze kushukuru, kabla hujalala mshukuru Mungu kwa mchana mzima na kabla hunakiacha kitanda upambazuke na Muumba wako.

Ninayofurahi kuona malengo yangu yanaelekea kukaa sawa, nina mpango wa kufungua kituo cha kusaidia watoto yatima, na nawashukuru wafuatao kwa kukubari kujiunga ili kuniwezesha kufanya hivyo.

Mats
Nancy
Anti. Fides
Antoniette


Nawashukuru kwa kubari kuwa member na naimani kituo kitasimama muda si mrefu. asanteni



SimaOmkama, ni jina tarajiwa la kituo cha kulelea watoto yatima kitakachokuwa katika wilaya ya karagwe nchini Tanzania. SimaOmkama ni neno la kihaya manake Shukuru Mungu. Kutokana na maisha niliyokulia kama mtoto yatima, najua shida na matakwa ya watoto yatima. Naimani nawe msomaji kama hukuguswa hili kwa mwili basi litakuwa limekugusa hata kwa macho, kuwaona watoto yatima wakihangaika mitaani, hakuna aliyependa kuishi maisha hayo ni shida tu namatatizo ya ulimwengu. Hivyo nimeamua kufungua kituo cha kusaidia watoto yatima. Hii ni kutokana na mme wangu pia kuniunga mkono kwani ingekuwa vigumu bila yeye. Zaidi nahitaji wanachanma( Members) ili niweze kupata misaada serikalini na kwa watu binafsi. Kwa moyo mmoja nilikuwa nakuomba uwe mwanachama kwa mchango wa 100kr kwa mwaka na Mungu atakubariki.

Asante sana. Renatha

Kwa kukubari kwako naomba ujaze form hii ili niweze kuziwakilisha kwa wakubwa, na iwapo kuna mikutano au mipango yoyote iwe vyepesi kuwasiliana.



Jina kamili la mwanachama…………………………………………
Anuani ya Mwana chama……………………………………………
Namba ya simu ya mwanachama……………………………………
Email ya mwanachama……………………………………………...
Tarehe ya kujiunga………………………………………………….

Sahihi ya mwanachama……………………………


Natanguliza shukurani na Mungu akubariki sana.

No comments:

Post a Comment