Wednesday 14 October 2009

Upumzike salama mwalimu Nyerere

Leo ni siku ambayo siwezi kuisahau maishani mwangu. tarehe 14 october. Nakumbuka mimi na wanafunzi wenzangu tulikuwa tukiomba sala Nyerere hasife hii tarehe lakini ikashindikana akafa. Tulikuwa tunamaliza darasa la saba ilikuwa siku ya sherehe. Tulizuiwa tusipige ngoma wala mziki, basi wapiga mziki tulokuwa tumela tumewakodisha walikula pesa yetu tu bure. Duh kweli nimekuwa kubwa miaka 10 sasa tangu nimalize darasa la saba ahhah lakini bado ninasoma tu.

Upumzike salama mwalimu daima ifikapo siku kama ya leo ntakukumbuka na naimani wote tuliomaliza darasa la saba au asilimia 90 tuliguswa sana na kifo cha mwalimu.

Tuesday 13 October 2009

Unene unapokuvamia







Jamani mwenzenu nilivamiwa na unene baada ya kupata mimba.
Wakati niko bk miezi 6 kbl sijaolewa nilikuwa hivi(Picha namba moja kutoka chini)

nikajitupa gym kidogo (Picha namba 2)

Nilipojifungua nkawa hivi (Picha namba 3)
Kuona nimekuwa hivi kidogo nikawa nimépunguza mazoezi nikafanya kula tu nikarudi tena nikawa hivi (picha namba nne) hivi sasa niko hivi hapo utuonapo famili ila nataka nipungue kidogo tena so nimeanza gym tena, vifaa vichache ninavyo home ila nashindwa kufanya mwenywe so nimeamua niende gym mwezi hivi ili niweze kujijengea mazoea.

Nahunganika na dada Dina kupunguza miili hii make mili mikubwa hifadhi za magonjwa.

Monday 31 August 2009

Namshukuru Mungu

Binadamu sisi niwasahaulifu sana. Utakuta mtu anaamka asubuhi anakurupuka kitandani mbio bila hata kumwomba Mungu ulinzi wala kumshukuru Kwa ulinzi wote usiku ule alipokuwa ameuchapa usingizi. Binadamu tujifunze kushukuru, kabla hujalala mshukuru Mungu kwa mchana mzima na kabla hunakiacha kitanda upambazuke na Muumba wako.

Ninayofurahi kuona malengo yangu yanaelekea kukaa sawa, nina mpango wa kufungua kituo cha kusaidia watoto yatima, na nawashukuru wafuatao kwa kukubari kujiunga ili kuniwezesha kufanya hivyo.

Mats
Nancy
Anti. Fides
Antoniette


Nawashukuru kwa kubari kuwa member na naimani kituo kitasimama muda si mrefu. asanteni



SimaOmkama, ni jina tarajiwa la kituo cha kulelea watoto yatima kitakachokuwa katika wilaya ya karagwe nchini Tanzania. SimaOmkama ni neno la kihaya manake Shukuru Mungu. Kutokana na maisha niliyokulia kama mtoto yatima, najua shida na matakwa ya watoto yatima. Naimani nawe msomaji kama hukuguswa hili kwa mwili basi litakuwa limekugusa hata kwa macho, kuwaona watoto yatima wakihangaika mitaani, hakuna aliyependa kuishi maisha hayo ni shida tu namatatizo ya ulimwengu. Hivyo nimeamua kufungua kituo cha kusaidia watoto yatima. Hii ni kutokana na mme wangu pia kuniunga mkono kwani ingekuwa vigumu bila yeye. Zaidi nahitaji wanachanma( Members) ili niweze kupata misaada serikalini na kwa watu binafsi. Kwa moyo mmoja nilikuwa nakuomba uwe mwanachama kwa mchango wa 100kr kwa mwaka na Mungu atakubariki.

Asante sana. Renatha

Kwa kukubari kwako naomba ujaze form hii ili niweze kuziwakilisha kwa wakubwa, na iwapo kuna mikutano au mipango yoyote iwe vyepesi kuwasiliana.



Jina kamili la mwanachama…………………………………………
Anuani ya Mwana chama……………………………………………
Namba ya simu ya mwanachama……………………………………
Email ya mwanachama……………………………………………...
Tarehe ya kujiunga………………………………………………….

Sahihi ya mwanachama……………………………


Natanguliza shukurani na Mungu akubariki sana.

Sunday 23 August 2009

Kwa mara ya tena


haya wapendwa miss universe isha anza tukae mkao wa kula.

Kila la Kheri OuR DaDa Illuminata

NI masaa manne yamebakia niruke na kudondosha laptop yangu kwa furaha hasa ntakapo mwona dadatu Illuminata akilibeba taji la miss Universe 2009. Wadau kaeni mkao wa kula naamka kwa ajili yangu na nyie.

Love you.

Kila la Kheri dda Illuminata

Friday 21 August 2009

My Mwana hair do!

hapa my Mwana akipozi na wenzie

my Mwana hapendani mtu amguse kichwani isipokuwa mama, so huwa namfunga hivi si unajua tena, wazazi tusiwasahau wanetu afu si tunatokomea salon. Hapo kakasirika mtu fulani alikuwa akimsaidia kuzifunga.

Tuesday 4 August 2009

USIKU HUU NIMEKOSA USINGIZI ILA NIMEPATA HILI

Ee Mungu u mwema, leo nimekosa usingizi nikasema ngoja niingie katika internet nilichokikuta hakika kimeifanya roho yangu itajirike ghafla, wimbo pia umenifanya ninenepe ghafla.

Naomba tushiriki wote wapendwa, kama imani yako imeshuka naimani itapanda.

enjoy

SIMLIZI (UPENDO WA MAMA

Habari za leo na karibu katika kigoda chako tayari kunisikiliza leo nimekuletea nini, ni tarehe moja mwezi wa saba mwaka 2009 saa kumi na mbili na dakika 26 kwa saa za skandinavia na saa moja za kibongo. Namshukuru Mungu kunionyesha siku ya leo Namshukuru Mungu kwa kunipa mtoto BYERA ambaye leo ninasherekea sikukuu ya kuzaliwa kwake miaka mitatu na masaa dunia, Asante Mungu. Leo nataka niongelee juu ya UPENDO WA MAMA, Kama rafiki yangu mpendwa alivyonishauri, ni rafiki nimpendaye sana na sijui kama itakuwaje… Nilimuuliza siku moja nikitafuta ushauri wa hadithi gani nitunge akaniambia nitunge juu ya upendo wa mama, sasa nafanya hivyo, najisikia kichwani kitu kimekaa tayari kuandikwa. Haya karibuni.
 
 
 
Je kati yangu na wewe ninani alipokuwa mdogo angependa kutoka shule akapokelewa na maneno km haya, mbwa wewe mbona umechelewa ulipitia wapi, shika ndoo hapo ukimbie kisimani ukateke maji kisha uwapikie wadogo zako chakula, mi naenda kwa mama koku kumjulia hali, kwanza nakueleza we nani, fanya haraka mbona unanitumbulia macho kama mjusi kabanwa na mlango, nasema timua. Bila hata ya kupewa chakula, kupewa muda wa kupumzika hata kumuona mdogo wako mwenye umri wa miaka 5 mliyeondoka wote asubuhi wakati anaenda kwenye shule yake ijulikanayo kama vidudu au chekechea.
 
Natambua kila mmoja wetu angetamani kupokelewa na upendo na tabasamu la kutosha pindi atokapo shule, kuulizwa mwanangu ilikuwaje, leo umesoma nini na kadharika. Kwa ukarimu kuisikia sauti ya mama yako mzazi ikikwambia karibu mtoto mzuri, nipe busu kisha ukavue nguo za shule, mi ngoja nikakuandalie chakula ule kisha upumzike kidogo. Hakika huo UPENDO wa namna hiyo unapatikana asilimia 100 kwa mtu mmoja aitwaye MAMA.
Mwanamke kama mwanamke naomba utambue kwanza kabla ya kuendelea kuwa uchungu ulioupata wakati unajifungua KAMGISHA AU KAGEMLO ni ule ule alioupata MAMA KOKU wakati akiwazaa KOKU na NDYAMKAMA. Hauna uzito tofauti na wako wala hauna rangi. Hii ilitokana na EVA kulila TUNDA alilokatazwa na Muumba wetu kwamba asile, na tokea hapo MUNGU alisema wewe mwanamke utazaa kwa uchungu. Hivyo uchungu huo niwakila mwanamke azaaye so SHOGA zangu msiwe na roho za kwa nini nakujiona watoto wenu ndio wanafaa. Haya karibu kigodani.

Itaendelea...

UJUMBE WA LEO: Kutoa ni moyo si utajiri, saidia yatima, mjane, maskini yeyote aliyekaribu yako, na MUNGU ATAKUBARIKI. Nawapenda

Friday 17 July 2009

yatima ni mwanao mpenzi

habari za leo??

Ndugu zangu wapendwa leo nimeamua kufungua homepage ambayo itahusu watoto yatima. Napenda wapendwa kote duniani mtakaweza kuisoma blog yangu, mjawe na roho za huruma na kuwapenda watoto yatima. karibu tushirikiane kuwapa UPENDO wa dhati kwani nao wangependa kuishi na wazazi wao ambao kwa namna moja au nyingine hawako nao tena na hawategemei kuwa nao mpaka Yesu arudi. karibu